BAADA ya siku 15 kupita kupisha kalenda ya FIFA ya michezo ya kimataifa, Ligi Kuu ya NBC inarejea tena Leo Septemba 15 kwa michezo mitatu kuchezwa kwenye mikoa tofauti.
Mchezo wa mapema utachezwa Saa 8:00 mchana kati ya KMC na JKT Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es salaam huku timu zote mbili zikipoteza kwenye michezo yao iliyopita kwa idadi sawa ya mabao matano.
Mchezo wa pili utachezwa kati ya Tabora United na Tanzania Prisons saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Ali hasssan Mwinyi, Tabora huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa Tabora United kucheza katika uwanja wao wa nyumbani baada ya kupanda daraja msimu huu.
Dodoma Jiji watakuwa nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma saa 1:00 usiku huku Mtibwa ikiwa haijashinda mchezo wowote na Dodoma ikipoteza mchezo uliopita kwa mabao 2-0 dhidi ya Simba.