Mzunguko wa sita wa Ligi Kuu ya NBC umetamatika huku vita ya pasi saidizi za mabao ikionekana kuanza kukolea kutokana na namna ambavyo wachezaji wanapambana kuweza kukusanya pasi hizo.
Libasse Gueye wa Simba ndie kinara wa mbio hizo akifanikiwa kuweka pasi saidizi tano ndani ya michezo sita ambayo timu hiyo ishacheza hadi sasa.
Hussein Zakouani wa Young Africans, Jeancy Mboma wa Singida Black Stars ndio wachezaji wanaofuatia kwa pasi nyingi ikiwa wameweza kutoa pasi saidizi tatu kila mmoja kwa timu zao ndani ya michezo mitano ambayo timu hizo zimeshacheza.
Yusuph Adam wa Singida Black Stars, Vicent Abubakar wa Geita Gold, Ani Elijah wa TRA United, Albert Kangwanda na Chadrack Boka wa Young Africans, Hassan Mubiru wa Azam na Denis Mushi wa Polisi Tanzania wamefanikiwa kuzipatia timu zao pasi saidizi mbili kila mmoja hadi sasa.
Ligi Kuu ya NBC inatarajiwa kuendelea tena Oktoba nane ikiwa ni baada ya mapumziko ya ratiba kalenda ya Fifa na utakuwa ni mzunguko wa saba wa Ligi hiyo.