LIGI ya Championship ya NBC inazidi kunoga ikiwa ni mzunguko wa pili wa Ligi hiyo iliyoanza Septemba 10 ikihusisha timu 16 kutoka mikoa mbali mbali.
Mzunguko wa pili unaanza leo kwa michezo miwili ambapo timu ya Mbeya Kwanza itakuwa mwenyeji wa timu ya Tanzania Prisons katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora na mchezo huo utakuwa mbashara kupitia chaneli ya Fifa+ huku Stand United ikiumana na timu ya Kigamboni United katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Kesho michezo miwili itachezwa pia ambapo Gunners itaikaribisha timu ya Bandari katika uwanja wa Jamhuri Dodoma ambapo mchezo utakuwa mbashara kupitia chaneli ya Fifa+ huku Mtibwa Sugar itacheza na Mbuni katika uwanja wa Manungu na mchezo huo utakuwa mbashara chaneli ya Ligikuu Tv kwenye mtandao wa Youtube.
Septemba 20 michezo minne itachezwa ambapo Transit Camp itaumana na TMA kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam huku pia mchezo huo uutaruka mbashara kwenye chaneli ya mtandao wa Youtube ya Ligikuu Tv.
Bigman dhidi ya KMC kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga , Songea United dhidi ya Rhino Rangers kwenye uwanja wa Maji Maji, Ruvuma na KenGold dhidi IAA katika uwanja wa Manispaa ya Chunya mkoani Mbeya.