LIGI Kuu ya NBC itaendelea leo kwa michezo miwili itakayochezwa katika mikoa ya Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine.
Mchezo wa kwanza utakuwa saa 8:00 mchana ambapo timu ya Pamba Jiji ya Mwanza itaialika timu ya Coastal Union ya Tanga katika ‘dimba’ la Kirumba.
Pamba Jiji inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikicheza michezo 12 ikishinda minne, sare tano na kufungwa mitatu huku ikikusanya alama 17.
Coastal ipo nafasi ya 12 katika msimamo ikicheza michezo 12 ikishinda miwili, sare tano na kufungwa michezo mitano huku ikikusanya alama 11.
Mchezo wa pili leo utakuwa majira ya saa 10:15 alasiri ambapo timu ya Tanzania Prisons itaialika timu ya Mashujaa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Prisons ipo nafasi ya 15 ikiwa imekusanya jumla ya alama nane ikiwa imeshinda michezo miwili, sare mbili na kufungwa michezo sita.