MASHUJAA YAPANDA KILELENI LIGI KUU YA NBC.

 

LIGI Kuu ya NBC imeendelea leo Agosti 17 kwa mchezo mmoja kuchezwa kati ya Mashujaa na Dodoma Jiji katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma na kumalizika kwa Mashujaa kuibuka na ushindi wa bao 1.

Bao hilo la kwanza kwa msimu wa 2024/25 limepatikana baada ya golikipa wa Dodoma Daniel Mgore kujifunga.

Ushindi huu unaipandisha Mashujaa hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 huku Dodoma Jiji ikishuka hadi nafasi ya mwisho kwenye msimamo.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho Agosti 18, kwa michezo miwili mchezo wa mapema saa 8:00 mchana utazikutanisha KenGold dhidi ya Singida Black Stars kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya huku mchezo wa pili saa 10:15 alasiri ukizikutanisha Simba dhidi ya Tabora UTD kwenye uwanja wa KMC, Dar es salaam.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *