LIGI Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 inaanza rasmi leo Agosti 16 kwa mchezo mmoja kuchezwa kati ya Pamba Jiji na Tanzania Prisons saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Pamba Jiji inarejea ligi Kuu na kucheza mchezo wake wa kwanza leo baada ya takribani miaka 23 kupitia tangu kushiriki Ligi hiyo.
Jumla ya michezo 240 itachezwa sawa na michezo 30 kwa kila timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC na michezo yote itarushwa mubashara na Azam Tv lakini pia unaweza kusikiliza matangazo ya redio kupitia TBC FM.