MPANZU KINARA WA KUPIKA MABAO YA LIGI KUU YA NBC.

 

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Elie Mpanzu, ameendelea kuthibitisha ubora wake katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/26 baada ya kuongoza orodha ya wachezaji wenye pasi nyingi za mabao kufikia sasa akiwa ametoa tisa (9).

Mpanzu amekuwa mhimili muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Simba , akichangia si tu kwa ubunifu wa kutengeneza nafasi za mabao bali pia kwa ushirikiano mzuri na washambuliaji wa timu hiyo, jambo lililoifanya Simba kuendelea kuwa na ushindani mkubwa katika mbio za ubingwa.

Anayemfuatia kwa karibu ni kiungo wa Azam, Feisal Salum mwenye pasi nane (8).

Feisal ameendelea kuonyesha kiwango cha juu msimu huu kwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa wenzake.

Katika nafasi ya tatu kuna kundi la wachezaji wanne wenye saba (7) kila mmoja, hawa ni Allan Okello wa Young Africans, Iddi Selemani wa Azam , Clatous Chama wa Simba na Zabona Mayombya wa Pamba Jiji.

Orodha hiyo inakamilishwa na wachezaji wawili wa Young Africans ambao ni Duke Abuya na Maxi Nzengeli wenye sita kila mmoja.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *