TIMU za Simba na Yanga zimeandika rekodi mpya ya kuwa timu mbili kutoka Tanzania zilizofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye msimu mmoja.
Yanga imefuzu hatua hiyo baada ya kuifunga Al-Merrikh ya Sudan kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0 huku wakishinda michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini.
Simba imefuzu baada ya kuitoa Power Dynamos ya Zambia kwa faida ya bao la ugenini baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao matatu katika matokeo ya jumla.
Simba itaanza michuano ya msimu huu ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kutolewa hatua ya robo fainali dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco msimu uliopita huku Yanga ikipoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger ya Algeria.