Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Nassor Idrissa, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Kocha Msaidizi wa Klabu ya Pamba Jiji, Themi Felix kilichotokea Oktoba 17, 2026 mkoani Mwanza
Kwa niaba ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Mwenyekiti ametoa pole kwa uongozi wa timu,wachezaji, benchi la ufundi, familia nzima ya Pamba Jiji na wadau wote wa mpira wa miguu kwa ujumla kufuatia msiba huo mzito.
Aidha, ametoa pole za dhati kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huo, akiwataka kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
“Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Themi Felix. Tunatoa pole kwa familia ya Pamba Jiji na wote walioguswa na msiba huu, Tunaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na tunawaombea faraja na nguvu ya kuhimili pengo hili kubwa,”amesema Nassor Idrissa.
Themi Felix alifariki katika hospitali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza alipokua Akipatiwa matibabu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
Imetolewa na;
Idara ya Habari na Mawasiliano
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
Oktoba 18, 2026.