WARATIBU WA MICHEZO (GC) WASISITIZWA KUWAJIBIKA.

LEO Agosti 12, 2024 Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imeendesha semina ya siku moja kwa waratibu wa michezo (Match General Coordinators) kuelekea msimu mpya wa 2024/2025.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Almasi Kasongo amewasisitiza waratibu wa michezo kuwajibika kwenye kazi zao za msingi.

“Kikubwa cha kuwaambia leo ni uwajibikaji, nyinyi ni watu muhimu sana katika kuhakikisha mchezo unachezwa, lakini kuna wengi ambao mnatuangusha licha ya wachache kati yenu kufanya vizuri” alisema kasongo.

Miongoni mwa yale yaliyowasilishwa katika semina hiyo ni Ulinzi na Usalama viwanjani, Shughuli za habari kabla na baada ya mchezo na Kanuni za Ligi.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *