MZUNGUKO wa 23 wa Ligi Kuu ya NBC umeendelea kwa mchezo mmoja uliochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya majira ya saa kumi alasiri.
Mchezo ulianza kwa timu zote kusomana kwa kuwa zilikuwa zinahitaji kupata alama tatu mhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi.
Iliwachukua dakika 21 kwa Mashujaa kupata bao la kwanza kupitia mchezaji Jafari Kibaya ambapo dakika ya 26 mchezaji wa Mashujaa, Yusuf Dunia, alijifunga na kufanya mchezo kusomeka 1-1 matokeo yaliyobaki mpaka mwisho wa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa ambapo dakika ya 47 mchezaji wa KenGold, Mishamo Daudi, aliiongezea timu yake bao la pili kabla ya Ally Nassor wa Mashujaa kuongeza bao la pili kwa mashujaa hivyo ubao kusomeka 2-2 mpaka mwisho wa mchezo.
KenGold walifikisha alama 16 wakiwa nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC huku Mashujaa wakifikisha alama 24 wakiwa nafasi ya 10.
Mchezaji wa Mashujaa,Ally Nassor ‘Ufudu’ alitangazwa kuwa nyota wa mchezo huo.Ligi Kuu ya NBC itaendelea leo kwa michezo mitatu.