MZUNGUKO wa 24 wa Ligi Kuu ya NBC utaendelea kushika kasi ambapo michezo mitatu itachezwa katika mikoa ya Kagera,Dar es Salaam na Mbeya hivyo kufanya mbio za ubingwa kuzidi kufikia mahali patamu zaidi kwani mmoja anapambana angalau apate alama ili aweze kubeba ubingwa ama aendelee kubaki msimu ujao .
JKT Tanzania ambayo ipo nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC itakuwa mwenyeji wa Dodoma Jiji iliyopo nafasi ya nane katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni Dar es Salaam majira ya saa kumi jioni.
KenGold iliyopo nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC itakawakaribisha timu ya Azam katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya majira ya saa kumi jioni huku Kagera Sugar atakuwa mwenyeji wa Coastal Union katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera majira ya saa moja usiku.
Kwa upande wa Ligi ya Championship ya NBC timu ya Songea United itaikaribisha timu Biashara United katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma majira ya saa kumi jionI ikiwa ni mzunguko wa 25 wa Ligi hiyo.