LIGI ya NBC Championship imeendelea leo Januari 6, kwa michezo minne kupigwa kwenye mikoa mitatu tofauti.
Mkoani Pwani michezo miwili ilipigwa kwenye uwanja wa Mabatini huku mapema saa 8:00 mchana Pan African waliwaalika Copco na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao moja, saa 10:00 alasiri Green Warriors wakawaalika Mbeya City na kumalizika kwa suluhu.
Polisi Tanzania wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani ushirika mkoani Kilimanjaro saa 8:00 mchana wakawakaribisha Mbeya Kwanza na kuibuka na ushindi wa bao moja.
Mkoani Shinyanga saa 10:00 alasiri Stand United ikawakaribisha TMA kwenye uwanja wa Mwadui Complex na Stand United kukubali kichapo cha mabao 1-6.
Kwa matokeo hayo TMA wanapanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na jumla ya alama 33 baada ya michezo 16.