Author: Yahaya Abushehe

JKT YASALIA LIGI KUU YA NBC, TABORA KUIVAA BIASHARA UNITED.

 

JKT Tanzania imefanikiwa kubakia Ligi Kuu ya NBC baada ya hii Leo kutoka suluhu na Tabora United kwenye mchezo wa pili wa mtoano hivyo JKT Tanzania kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-0.

Mchezo wa kwanza wa mtoano uliochezwa kwenye uwanja wa Ali hassan Mwinyi mkoani Tabora ulishuhudia wenyeji Tabora United wakikubali kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya wageni wao JKT Tanzania.

Sasa Tabora United itakwenda kujaribu bahati yao ya kusalia Ligi Kuu ya NBC kwa kuwavaa Biashara United iliyokuwa ikishiriki Ligi ya NBC Championship, mchezo wa kwanza utachezwa Juni 12 mkoani Mara huku mchezo wa pili utachezwa Juni 16.

Mshindi wa jumla kwenye michezo hiyo miwili atashiriki Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 na atakayepoteza atashiriki Ligi ya NBC ya Championship.

GEITA GOLD YAUNGANA NA MTIBWA NBC CHAMPIONSHIP.

 

BAADA ya pazia la Ligi Kuu ya NBC Msimu wa 2023/2024 kumalizika rasmi jana Mei 28 na kushuhudia Geita Gold ikiungana na Mtibwa Sugar kushuka daraja na mwakani kushiriki Ligi ya NBC Championship.

Geita Gold ilikusanya alama 25 kwenye michezo 30 ikishinda michezo mitano ikifungwa 15 na kupata sare michezo 10 ambapo alama hızo zilishindwa kuwabakisha Ligi Kuu ya NBC msimu ujao.

Mtibwa Sugar ndio ilikuwa ya kwanza kushuka daraja kwenye mzunguko wa 29 baada ya kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Mashujaa.

Timu za JKT Tanzania na Tabora United zitacheza mchezo wa Mtoano kutafuta nafasi ya Kubaki Ligi Kuu ya NBC msimu ujao wa 2024/2025, atakayefungwa kwenye mchezo huo atakutana na Biashara United ya NBC Championship kutafuta nafasi ya kushiriki Ligi Kuu ya NBC msimu ujao.

LIGI KUU YA NBC KUENDELEA LEO

LIGI KUU YA NBC KUHITIMISHWA LEO.

 

Ligi Kuu ya NBC inafika tamati Leo Mei 28 kwa michezo nane ikihusisha timu zote 16 Zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC kupigwa kuanzia saa 10:00 alasiri kwenye mikoa saba tofauti.

Michezo ya leo itaamua hatma ya baadhi ya timu ikiwemo vita ya nafasi ya pili, nani kushuka daraja, nani kucheza mtoano (Playoff) na vita ya ufungaji bora.

Nafasi ya pili inapambaniwa na Timu za Azam na Simba ambapo Azam Ina alama 66 kwenye michezo 29 sawa Simba wakitofautiana kwenye mabao ya kufunga na kufungwa ambapo Azam akiwa na utofauti mkubwa wa mabao (40) kuizidi Simba (32).

Anayeshika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya NBC anapata nafasi ya kuiwakilisha Nchi kwenye michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika.

Vita ya kushuka daraja na Kuungana na Mtibwa Sugar iliyotangualia Ligi ya NBC ya Championship ipo mikononi mwa Geita Gold na Tabora United ambapo Geita ikiwa na alama 25 huku Tabora United ikiwa na alama 27.

Geita inahitaji ushindi na kuomba Tabora ipoteze ili kufikisha alama 28 ambazo zitaipa nafasi ya kushiriki hatua ya mtoano (Playoff) , Tabora inahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kucheza mtoano (Playoff).

Kila nafasi ambayo timu itamaliza kwenye Ligi Kuu ya NBC ina zawadi ya fedha kutoka kwa mdhamini mwenye haki ya matangazo ya Ligi Kuu ya NBC Azam Tv.

MTIBWA SUGAR YASHUKA DARAJA.

 

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa michezo nane inayohusisha timu zote 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC kuchezwa kuanzia saa 10:00 alasiri kwenye mikoa Saba tofauti.

Baada ya kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Mashujaa, Rasmi Mtibwa Sugar imeshuka Daraja na itashiriki Ligi ya NBC Championship msimu ujao wa 2024/2025.

Ligi Kuu ya NBC itahitimishwa Mei 28 kwa michezo nane inayohusisha timu zote 16 kuchezwa kwa muda mmoja kuanzia saa 10:00 alasiri.

BIASHARA YAIANZA VEMA VITA YA KUPANDA LIGI KUU YA NBC.

 

MCHEZO wa kwanza wa mchujo wa timu za NBC Championship kupanda Ligi Kuu ya NBC Kati ya BIashara United na Mbeya kwanza umemalizika kwa Biashara United kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya kwanza.

Mabao ya Biashara United yamefungwa na Abeid Othman dakika ya 22 na Boban Bogere dakika ya 34 na Kuifanya Biashara United kuondoka na ushindi huo muhimu kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Mchezo wa pili wa mtoano utachezwa Mei 26 saa 10:00 alasiri katika uwanja wa Nangwanda sijaona mkoani Mtwara ukiwa uwanja wa nyumbani wa Mbeya kwanza.

Mshindi wa jumla wa michezo hii atacheza na timu iliyofungwa kwenye mchezo utakaozikutanisha timu zilizoshika nafasi ya 13 na 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC na mshindi wa mchezo huo kushiriki Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025.