Author: Yahaya Abushehe

Nassor Idrissa

NASSOR IDRISSA MWENYEKITI MPYA BODI YA LIGI.

NASSOR Idrissa ‘Father’ amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) baada  ya kupata kura saba (7) dhidi ya kura sita (6) za mpinzani wake CPA Hosea Lugano kwenye uchaguzi uliofanyika jana Novemba 29, 2025 katika Hotel ya Golden Tulip, Masaki Jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Nassor alisisitiza chini ya utawala wake atahakikisha haki inapatikana kwa kila timu bila kujali ukubwa wa timu, hususani maamuzi yanayotolewa ndani ya Dakika 90 za mchezo.

Katika Hatua nyengine Hassan Muhsini Mwenyekiti wa Coastal Union amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ambapo katika nafasi hiyo hakuwa na mpinzani hivyo kupitishwa kwa kura ya ndio wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

Pia Japhet Makau Rais wa Fountain Gatena Gilbert Nkolonko Mwenyekiti wa Mbeya City wamechaguliwa kuwa wajumbe wawakilishi wa klabu za Ligi Kuu ya NBC huku Ahmed Gao wa Bigman na John Ndumbaro wa Mbeya City wakichaguliwa kuwa wajumbe wawakilishi wa klabu za Ligi ya Championship ya NBC wakati huohuo Azim Khan wa Dar City akichaguliwa kuwa mjumbe muwakilishi wa klabu za First League.

kagera sugar kupindua meza

KAGERA SUGAR KUPINDUA MSIMAMO LEO ?

Kagera Sugar inashuka Dimbani hii leo Novemba 22 kuwakabili Polisi Tanzania kwenye muendelezo wa Ligi ya Championship ya NBC 2025/2026 mchezo utakao chezwa kwenye uwanja wa Kaitaba kuanzia saa 10:00 alasiri.

Kagera Sugar inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikiwa na alama 13 sawa na Geita Gold inayoshika nafasi ya kwanza wakitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Kwa upande wa Polisi Tanzania ina jumla ya Alama 10 baaada ya michezo mitano ya Ligi ya Championship ya NBC ikishinda michezo mitatu, kufungwa mmoja na kutoka sare mchezo mmoja.

UShindi kwenye mchezo wa leo unaweza kuwapeleka ‘Wana Nkurukumbi’ Kagera Sugar kwenye kilele cha Ligi ya Championship ya NBC ikiwa mpinzani wake wa Karibu Geita Gold akipata matokeo mengine tofauti na ushindi.

Mkoani Tanga African Sports itaikaribisha Geita Gold kinara wa Ligi ya Championship ya NBC kwenye uwanja wa Mkwakwani mchezo utakaoanza saa 10:00 alasiri, Mchezo huu utarushwa Mubashara ‘Live’ kupitia FIFA+.

NANI KUSHIKA USUKANI WA KILELE CHA MSIMAMO WA LIGI KUU YA NBC LEO ?

 

LIGI KUU ya NBC inarejea Leo Novemba 8 kwa michezo miwili kupigwa kwenye mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam baada ya kusimama kwa muda kwasababu ya changamoto za kiuendeshaji zilizotokana na sababu za kiusalama na Miongozo yake.

Mkoani Mwanza Pamba Jiji itaialika Singida Black Stars saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Pamba inashika nafasi ya pili (2) kwenye Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikijikusanyia alama 8 kwenye michezo mitano huku Singida BS ikiwa nafasi ya nane (8) na alama zake sita baada ya michezo miwili.

‘Wazee wa kichapo cha Kizalendo’ JKT Tanzania itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye uwanja wa Mej. Jen Isamuhyo saa 1:00 Usiku. Huu ni mchezo wa tatu wa Ligi Kuu ya NBC kuchezwa usiku katika uwanja huo.

JKT Tanzania inaingia kwenye mchezo huu ikiwa imefunga mabao Saba na kuruhusu mabao sita kwenye michezo yake mitano iliyocheza, sawa na kusema imefunga na kuruhusu bao katika kila mchezo wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2025/2026 huku Simba ikifunga mabao sita na kutoruhusu bao lolote kwenye michezo miwili iliyocheza.

Alama tatu kwa kila timu kwenye michezo ya Leo zinaweza ipa timu yoyote nafasi ya kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026.

SINGIDA BLACK STARS YAPAA KILELENI MSIMAMO WA LIGI KUU YA NBC.

SINGIDA Black Stars imepanda kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Mashujaa kwenye uwanja wa KMC.

Bao pekee la Singida BS limefungwa na mchezaji Elvis Rupia raia wa Kenya dakika ya 45+5 ya mchezo.

Singida Black Stars
Singida Black Stars

Ushindi huo unaifanya Singida BS kufikisha alama sita baada ya michezo miwili huku ikiwa haijaruhusu bao.

Mchezo wa pili ulipigwa saa 10:15 alasiri mkoani Mbeya uliozikutanisha Mbeya City dhidi ya Young Africans kwenye uwanja wa Sokoine na kumalizika kwa Suluhu.

Mbeya City Vs Young Africans
Mbeya City Vs Young Africans

Mchezaji Baraka Filemon  wa Mbeya City alitajwa Kama Mchezaji Bora wa mchezo huo kutokana na mchango mkubwa aliotoa kwa timu yake kwenye mchezo huo.

PAZIA LA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026 KUFUNGULIWA LEO.

PAZIA la Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 linafunguliwa leo kwa michezo miwili kuchezwa kwenye viwanja vya KMC, Dar es salaam na Mkwakwani, Tanga.

Mchezo wa Kwanza kwenye uwanja wa KMC Complex utazikutanisha timu za KMC ya Dar es salaam na Dodoma Jiji ya Dodoma.

 

 

KMC COMPLEX – DAR ES SALAAM

 

 

Wakizungumza Kuelekea mchezo huo makocha na wachezaji wa timu zote mbili wameonesha kuwa tayari kwa mchezo huo huku wakiwa na shauku kubwa baada ya kuwa timu za kwanza kucheza kwa msimu wa 2025/26.

 

 

msimu wa 2025/2026

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kwa upande wa KMC waliwakilishwa na Kocha Mkuu Marcio Maximo na Mchezaji Daruweshi Saliboko huku Dodoma Jiji wakiwakilishwa na Kocha Mkuu Vincent Mashami na Nahodha Augustino Nsata.

Mchezo wa pili utapigwa saa 1:00 usiku kati ya Coastal Union na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga ambapo Coastal Union ilimaliza msimu wa 2024/2025 ikiwa nafasi ya nane huku Dodoma Jiji ikimaliza nafasi 12.