Author: Yahaya Abushehe

TANZANIA KUIVAA MOROCCO ROBO FAINALI CHAN.

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itaivaa timu ya Taifa ya Morroco kwenye hatua ya Robo Fainali ya michuano ya CHAN 2024 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 22, 2025. 

Taifa Stars ilifika hatua hiyo baada ya kuongoza kundi B ikiwa na alama 10 baada ya kushinda michezo mitatu na kupata sare mchezo mmoja huku ikifunga jumla ya mabao matano na kuruhusu bao moja pekee.

Kwa upande wa Morocco ilifikia hatua hii baada ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi A lililoongozwa na Taifa jirani la Kenya.

Morroco ilishinda michezo mitatu na kupoteza mchezo mmoja hivyo kumaliza kwenye nafasi ya pili ikiwa na alama tisa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufika hatua ya Robo Fainali ya michuano ya CHAN kwenye historia ya ushiriki wake kwenye mashindano hayo.

KARIA MINNE TENA TFF.

KARIA MINNE TENA TFF.

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amethibitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF kuwa Rais wa Shirikisho hilo kwa kipindi kingine cha miaka minne katika uchaguzi wa TFF uliofanyika jana Agosti 16 Mkoani Tanga.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo Rais Karia alisisitiza watu kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizojitokeza huko nyuma.

“Nawashukuru leo mmenipitisha lakini twende tukafanye kazi, tuna hitaji taarifa kwenu na pia tutafatilia kwasababu tutakapofanya peke yetu huku juu chini hakufanyiki kitu hatuwezi kufanikiwa” alisema Rais Wallace Karia.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inampongeza Ndugu Wallace Karia na kumtakia kila la kheri kipindi kingine cha miaka minne ya majukumu yake.

 

 

 

MZIZE

TANZANIA YAANDIKA HISTORIA MPYA CHAN.

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya michuano ya CHAN2024 inayoendelea katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda na kuwa nchi ya kwanza kujihakikishia kucheza hatua hiyo ya Robo Fainali.

Stars imefika hatua hiyo baada ya jana Agosti 9, kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Madagascar hivyo kujikusanyia alama tisa (9) baada ya kushinda michezo yote mitatu iliyocheza kwenye kundi lake.

Mabao yote ya Stars yalifungwa na Clement Mzize dakika ya pili na ya 21, hii ni kwa mara ya kwanza Clement Mzize anaifungia Timu ya Taifa ya Tanzania kwenye mchezo wa kimashindano.

Na hii ni mara ya kwanza kwa Timu ya Taifa ya Tanzania kufuzu hatua ya Robo Fainali tangu kuanzishwa kwa mashindano haya ya CHAN.

TANZANIA YAANZA NA USHINDI CHAN 2024.

TANZANIA YAANZA NA USHINDI CHAN 2024.

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeanza vyema michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani CHAN 2024 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Burkina Faso.

Mabao ya Stars yalifungwa na Abdul Suleimani anaekipiga kwenye timu ya Azam ya Dar es Salaam kwa mkwaju wa penati huku la pili likifungwa na Mohammed Hussein aliyemaliza mkataba wake na timu ya Simba akimaliza kazi safi iliyofanywa na Iddy Selemani (Nado) wa Azam.

Mchezo huo ulitanguliwa na Shamra shamra za ufunguzi wa michuano hiyo ambao kwa upande wa burudani ziliongozwa na msanii wa Bongo Fleva Raymond Mwakyusa maarufu Kama ‘Rayvanny’.

Timu ya Tanzania inaundwa na ‘mastaa’ mbalimbali wanaocheza Ligi za ndani ikiwemo Ligi Kuu ya NBC na Ligi ya Championship ya NBC.

Tanzania itarejea tena uwanjani Jumatano ya Agosti 6, saa 2:00 usiku ikiivaa timu ya Taifa ya Mauritania.

NI VITA YA UBINGWA ‘DERBY’ YA KARIAKOO LEO.

 

‘DERBY YA MAAMUZI’ ndivyo unavyoweza kuuita mchezo wa watani wa Jadi ‘Kariakoo Derby’ ndani ya Ligi Kuu ya NBC unachezwa leo saa 11:00 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Huu ni mchezo wa kufunga Pazia la Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2024/2025 lakini pia ndio mchezo utakaotoa Bingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu huu wa 2024/2025.

Young Africans inahitaji alama moja pekee ili kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu huu kwa kuwa itafikisha alama 80 ambazo haziwezi fikiwa na timu nyengine yoyote.

Matokeo ya Ushindi ndio silaha pekee kwa Simba ili kuweza kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu huu wa 2024/2025, hii ni kutokana na utofauti wa alama Kati yake na timu inayoongoza Ligi Young Africans.

Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo uliopita huku ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na alama 79.

Mwamuzi wa kati kwenye mchezo huu ni Amin Mohammed Amin, mwamuzi msaidizi namba moja ni Mahmoud Ahmed Abo, mwamuzi msaidizi namba mbili Samil Gamal Saad na mwamuzi wa akiba ni Ahmed Mahrous Elghandour wote kutoka Misri.