BODI YA LIGI KUU TANZANIA (TPLB) KUPOKEA MABORESHO YA KANUNI ZA LIGI

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inautaarifu umma kuwa imeanza kupokea maoni ya maboresho ya Kanuni za Ligi kwa toleo la mwaka 2026. Maoni/mapendekezo hayo ya maboresho ya kanuni ni kwa ajili ya Ligi Kuu Ligi ya Championship na First League.

Lengo la zoezi hili ni kuboresha Kanuni za Ligi ili ziweze kutatua changamoto zilizojitokeza na zinazoweza kujitokeza katika msimu wa 2025/2026. Mchakato huu wa kupokea maoni utafanyika kwa kipindi cha majuma manne (4) na umefunguliwa rasmi Aprili 22, 2026.

Bodi inawakumbusha wadau wote kuwa kanuni bora ni msingi wa kuwa na ligi bora na maendeleo ya mpira wa miguu kwa ujumla, hivyo ushiriki wa kila mdau ni jambo la muhimusana.

Maoni ya maboresho ya kanuni yawasilishwe TPLB kabla ya Mei 22, 2026 kwa kupitia njia zifuatazo;

i. Barua pepe – maoni@ligikuu.co.tz

ii. Ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) au WhatsApp +255 758 500 222

iii. Kuwasilisha kwa mkono katika ofisi za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania zilizopo

ghorofa ya 14 kwenye jengo la NSSF (Mafao House), Ilala – Dar es Salaam.

3 comments

  1. tunataka team mashababiki wakifanya fujo wafungiwe hata mechi tatu mfululizo pasiapoa kuwa na mashabiki ili tukomeshe tabia mbovu za mashabIki kama kulusha makopo na vingine

  2. Kuwepo na sheria inayoipa timu alama tatu ikithibitika kwamba waamuzi wa mchezo hawakufuata sheria na kanuni katika maamuzi ya mchezo husika mf.timu A imenyimwa goli la wazi huku mwamuzi akionyesha kuwa ni offside wakati sivyo

  3. taitwa anunda mfalingundi mi napenda timu ikipetia mlango mwingine kuingia uwanjani ikatwe poindi

Join the Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *