TIMU ya Mbeya City imerejea rasmi Ligi Kuu ya NBC ambayo ni Ligi namba nne kwa ubora barani Afrika wakitokea Ligi ya Championship ya NBC baada ya kufanikiwa kufikisha alama 65 baada ya kuifunga timu ya Cosmopolitan mabao 5-0 huku ikiwa na mchezo mmoja ikiwa ni wiki moja baada ya Mtibwa Sugar kufanikiwa kurejea Ligi Kuu ya NBC.
Mbeya City ilishuka na sasa wamerejea rasmi huku ikiwa imeweka rekodi ya kufunga mabao mengi ksatika Ligi ya Championship baada ya kufunga mabao 63 katika michezo 29 ambayo timu hiyo imeshacheza mpaka sasa huku katika michezo yao 14 ya nyumbani wakishinda 11 na sare 3 na ugenini michezo 15 wakishinda michezo nane sare tano na kufungwa michezo miwili
Aidha timu hiyo imefanikiwa kufunga mabao 63 kuruhusu mabao 26 katika michezo timu hiyo iliyocheza huku wakiwa wamebaki na mchezo mmoja ili kuweza kutamatika kwa Ligi ya Championship ya NBC ambao pia utaamua nani bingwa wa Ligi hiyo kati ya Mtibwa Sugar wenye alama 68 au Mbeya City wenye alama 65.