Category: STORY

Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC 2025/2026

TAARIFA YA KAMATI YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA LIGI YA BODI YA LIGI KUU TANZANIA.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Machi 26, 2026 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Ligi Kuu ya NBC

Mechi Namba 85: Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC

Mashabiki wa timu ya Simba.

Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. 10,000,000 (milioni kumi) kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi wa mchezo tajwa hapo juu wakati wakitoka kiwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo huo.Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha miezi miwili ambapo Februari 25, 2026 mashabiki wa klabu hiyo walimrushia chupa za maji mchezaji wa klabu ya Dodoma Jiji, William Edgar wakati mchezo huo ukiendelea kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu na mazingatio ya kosa la kujirudia.

Mechi Namba 110: TRA United FC 0-0 Young African SC

Klabu ya TRA United ya mkoani Tabora imetozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la wachezaji wake kuonyeshwa kadi zaidi ya tano (5) katika mchezo mmoja, ambapo wachezaji hao walionyeshwa jumla ya kadi sita (6) kwenye mchezo tajwa hapo juu.Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 47:10 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Mechi Namba 126: Mtibwa Sugar FC 1-1 Young Africans SC

Golikipa wa Young Africans,Djigui Diarra.

Mchezaji Djigui Diarra wa klabu ya Young Africans amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kumshambulia mwamuzi wakati wa mchezo tajwa hapo juu, mara baada ya mchezo huo kumalizika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.3) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.Mchezaji Djigui Diarra wa klabu ya Young Africans ametozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kuonesha kidole cha kati wakati akitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo tajwa hapo juu.

Diarra ametenda kosa kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.4) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji, kwa sababu kitendo hicho kinaashiria matusi na dharau.Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.

Mwamuzi wa kati wa mchezo tajwa hapo juu, Gilbert Mrina kutoka Kilimanjaro,ameshushwa Daraja la Uamuzi kwa kosa la kushindwa kuchukua hatua stahili kwa mchezaji Djigui Diarra kwa kitendo chake cha utovu wa nidhamu (kumshambulia mwamuzi) kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni ya 42:1(1.6) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kuwa ni kosa la kujirudia ambapo mwamuzi Gilbert Mrina alitenda kosa la aina hiyo katika mchezo namba 65 wa Ligi Kuu ya NBC (Mbeya City vs Namungo) na akaadhibiwa kwa kufungiwa mizunguko mitatu (3).Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Mwamuzi msaidizi namba mbili (2) wa mchezo tajwa hapo juu, Abdulaziz Ally kutokaArusha, amefungiwa mizunguko mitano (5) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheriaza mpira wa miguu ambapo katika dakika ya 36 ya mchezo alinyoosha kibendera juu kuashiria kulikuwa na kosa la kuotea kabla ya mchezaji Emmanuel Mwanengo wa Young Africans kupokea pasi kutoka kwa Pacome Zouzoua. Hata hivyo, hakukuwa na kosa la kuotea kwa mujibu wa sheria za mpira wa miguu.Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwaWaamuzi.

Imetolewa na;

Idara ya Habari na Mawasiliano

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)

NBC CHAMPIONSHIP ‘YAFUKUTA’ MZUNGUKO WA 21.

Ligi ya NBC Championship imetimiza mzunguko wa 21 huku ushindani ukizidi kupamba moto, timu zikionyesha wazi dhamira ya kupigania kupanda daraja kwenda Ligi Kuu ya NBC msimu ujao na nyingine zikipambana kusalia ligi hiyo msimu ujao.

Katika hatua hii ya ligi, kila alama imekuwa ya thamani kubwa, huku timu za juu ambazo ni Geita Gold, Kagera Sugar,Mbeya Kwanza na Transit Camp zikionekana kuongeza kasi ili kujihakikishia nafasi za moja kwa moja za kupanda daraja na mapambano hayo yameifanya ligi kuwa na mvuto mkubwa zaidi, ambapo matokeo ya kila wiki yamekuwa yakibadilisha mwelekeo wa msimamo wa ligi hiyo.

Kwa upande wa katikati ya msimamo penye timu za Bigman yenye alama yenye alama 27 ikishika nafasi ya saba, KenGold inafuata ikiwa na alama 26 sawa na Songea United na Gunners inayoshika nafasi ya 10 ikiwa imekusanya alama 23 hali inaendelea kuwa ngumu kwa timu hizo ambazo zinajikuta zikihitaji ushindi mfululizo ili kuepuka kuingia kwenye hatari ya kushuka daraja na jambo hil limeongeza ushindani mkali, kwani tofauti ya pointi kati ya timu hizo ni ndogo sana.

Wakati huo huo, timu za ‘mkiani’ ambazo ni African Sports inayoshika nafasi ya 15 na Barberian inayoshika nafasi ya 16 zinapambana kwa nguvu zote kujiokoa, hali inayofanya kila mechi kuwa ya ushindani wa hali ya juu na presha imekuwa kubwa kwa wachezaji na benchi la ufundi, huku makosa madogo yakigharimu matokeo makubwa.

Ligi hiyo pia imeendelea kuwa jukwaa muhimu kwa wachezaji kuonyesha viwango vyao, ambapo baadhi yao kama Obrey Chirwa anayekipiga kwenye timu ya Kagera Sugar anayeongoza mbio za ufungaji na Ramadhan Karanje wa B19 aliyeibuka mchezaji bora wa mwezi Februari wameanza kuvutia macho ya klabu kubwa kutokana na kiwango wanachoonyesha uwanjani.

Kadri msimu unavyozidi kusonga mbele, wachambuzi wa soka wanaamini kuwa ushindani utaongezeka zaidi, hasa katika nafasi za juu zinazoongozwa na kinara Geita Gold zinazotoa tiketi ya kupanda Ligi Kuu ya NBC pamoja na zile za mkiani zinazohusisha mapambano ya kuepuka kushuka Ligi ya First League.

Kwa sasa, macho ya wadau wa soka yameelekezwa kwenye hatua zijazo za ligi hiyo iliyosimama kwa takribani mwezi mmoja, wakisubiri kuona ni timu zipi zitafanikiwa kuhimili presha na kuandika historia ya kupanda daraja mwishoni mwa msimu na zipi zitaweza kuamka na kusalia kwenye ligi msimu ujao.

SINGIDA YATAMBA UGENINI, DAR ‘DERBY’ HAKUNA MBABE LIGI KUU YA NBC.

 

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa timu ya Singida Black Stars kupata ushindi mnono wa mabao 4–1 dhidi ya Mbeya City ugenini katika mchezo uliochezwa mkoani Manyara kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara.

Mbeya City ilianza vizuri mchezo na kupata bao la kuongoza dakika ya 14 kupitia kwa mshambuliaji Vitalis Mayanga.

Hata hivyo, Singida Black Stars walirudi kwa nguvu na kusawazisha dakika ya 31 kupitia kwa Emmanuel Keyeh kupitia mkwaju wa penati na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare.

Kipindi cha pili kilikuwa cha Singida Black Stars ambapo iliongeza kasi ya mashambulizi na dakika ya 69 Mosi Ndumumwe aliifungia timu yake bao la pili kabla ya beki Ibrahim Imoro kufunga mabao mawili mfululizo dakika ya 72 na 86 na kuhitimisha karamu hiyo ya mabao kwa Singida.

Ushindi huo unaifanya Singida Black Stars kuendelea kujiweka kwenye hali nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC huku Mbeya City wakilazimika kujipanga upya kwa ajili ya michezo ijayo.

Mchezo mwingine ulipigwa saa 2 :30 usiku katika uwanja wa Benjamin william Mkapa ambapo mabigwa watetezi Young africans waligawana alama na Azam baada ya kutoka sare katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa na kasi kutoka kwa timu zote mbili

Katika mchezo huo kiungo mahiri wa Azam Feisal Salum aliibuka kuwa mchezaji bora wa mchezo huo kufuatia kiwango chake kizuri alichokionyesha uwanjani.

MAHESABU MAKALI ‘DAR DERBY’ LIGI KUU YA NBC LEO.

 

Ni vita ya mahesabu makali kwenye Mchezo wa ‘Derby’ ya Dar es salaam leo Machi 15, 2026 ambapo Azam FC itaialika Young Africans kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa saa 2:30 usiku.

Azam FC na Young Africans ndio timu pekee kwenye Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 ambazo hazijapoteza mchezo wowote hadi sasa katika michezo 13 timu hizo iliyocheza.

Kwenye eneo la ulinzi na ushambuliaji timu hizi zina namba nzuri zaidi kulinganisha na timu nyengine zinazoshriki Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Kwa upande wa upachikaji mabao Young Africans imefunga jumla ya mabao 31 mengi zaidi kuliko timu yoyote ndani ya Ligi Kuu ya NBC ikifuatiwa na Azam FC iliyofunga mabao 21.

Kwenye eneo la Ulinzi Young Africans imeruhusu mabao mawili pekee machache zaidi kuliko timu yeyote inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC ikifuatiwa na Azam FC iliyofungwa mabao manne pekee.

Ushindi kwa Azam FC utaifanya kufikisha alama 30 na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC lakini pia kupunguza ‘pengo’ la alama na Kinara wa Ligi Kuu ya NBC Young Africans kwa alama tano (5).

Ushindi kwa Young Africans utaifanya iendelee kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa kufikisha alama 38 na kuendelea kuweka pengo kubwa la alama na wapinzani wake wa karibu.

Tukutane Benjamin Mkapa saa 2:30 usiku tushuhudie kipute cha Ligi Kuu ya NBC.

YOUNG AFRICANS HAIKAMATIKI LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Young Africans ‘Wananchi’ imezidi kuchanja mbuga kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kushinda mchezo wa 11 Kwenye michezo 13 ikiwa haijapoteza hata mmoja na kutoa sare miwili pekee.

’Wananchi’ wameongeza ushindi huo baada ya kuifunga Tanzania Prisons iliyokuwa mwenyeji wa mchezo huo uliopigwa uwanja wa Jamhuri, Dodoma baada ya uwanja wao ‘mama’ wa Sokoine, Mbeya kufungiwa kupisha maboresho.

Laurindo Dilson ‘Depu’ aliandika bao lake la sita msimu huu likiwa bao pekee lililopeleka furaha kwenye mitaa ya ‘Jangwani’ baada ya mchezo uliopita Young Africans kutoa sare na mahasimu wao wakubwa timu ya Simba.

Young Africans wanaendelea kujichimbia kwenye ‘kilele’ cha Ligi Kuu ya NBC wakifikisha jumla ya alama 35 baada ya kucheza michezo 13 huku timu inayowafuata kwa karibu (JKT Tanzania) ikicheza michezo … zaidi ya ‘Wananchi’.

Ingawa Depu aliingia kwenye mchezo huo alifanikiwa kuondoka na tuzo ya mchezaji bora wa mchezo hii ni baada ya bao alilofunga na kiwango alichokionyesha kuipa alama tatu muhimu Young Africans ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC.