Category: STORY

COSMOPOLITAN, BIASHARA ZATAKATA NBC CHAMPIONSHIP LEO.

 

MZUNGUKO wa 17 Ligi ya NBC Championship umeanza leo kwa michezo miwili Kupigwa.

Cosmopolitan ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Mabatini mkoani Pwani ikaibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Copco.

Saa 10:00 alasiri Biashara iliwaalika TMA kwenye uwanja wa Karume, Mara na kumalizika kwa Biashara kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Biashara sasa Imepanda hadi nafasi ya pili ikiwa na alama 36 sawa na Ken Gold wakitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa na idadi ya michezo Biashara ikiwa na michezo 17 huku Ken Gold ikiwa na michezo 16.

BIASHARA, TMA NANI KUSHIKA USUKANI WA NBC CHAMPIONSHIP LEO ?

 

LIGI ya NBC Championship mzunguko wa 17 inaanza leo kwa michezo miwili kupigwa kwenye mikoa miwili.

Mapema saa 8:00 mchana Cosmopolitan itakuwa mwenyeji wa Copco kwenye uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.

Cosmopolitan ipo nafasi ya 14 katika msimamo wa NBC championship baada ya kukusanya alama 14 katika michezo 16 huku Copco ikiwa nafasi ya 15 na alama 12 katika michezo 16.

Mchezo wa mwisho leo utazikutanisha Biashara United dhidi ya TMA kwenye uwanja wa Karume, Mara saa 10:00 alasiri.

Mchezo huu unabeba hisia za watu wengi kutokana na timu itakayoshinda itapanda hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo Biashara ikishika nafasi ya tatu na alama 33 kwenye michezo 16 sawa na TMA huku timu hizo zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

SIMBA YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI.

Simba imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Singida FG kwa mikwaju ya penati 3-2 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Singida ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 11 ya mchezo likifungwa na mchezaji Elvis Rupia huku bao la kusawazisha la Simba likifungwa na mchezaji Fabrice Ngoma dakika ya 90+8.

Simba itakutana na Mlandege ambao ndiyo mabingwa watetezi wa kombe hilo katika hatua ya fainali itakayochezwa januari 13 katika dimba la New Amaan Complex.

TMA WANA UKUTA MGUMU NBC CHAMPIONSHIP.

 

TAYARI mabao 286 yamefungwa hadi hivi sasa kwenye Ligi ya NBC Championship baada ya mizunguko 16 ya Ligi hiyo kukamilika.

TMA ndiyo timu iliyofungwa mabao machache hadi hivi sasa ikifungwa jumla ya mabao 5 katika michezo 16 waliyocheza.

Ken Gold na Pamba ndiyo wanafuatia kwa kufungwa mabao machache wakifungwa mabao 10 kila mmoja kwenye michezo 16 waliyocheza.

Ruvu Shooting ndiyo timu iliyoruhusu mabao mengi zaidi wakiruhusu jumla ya mabao 34 kwenye michezo 16 waliyocheza

SINGIDA FG, SIMBA NANI KWENDA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI ?

 

HATUA ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi inamalizika leo januari 10 kwa mchezo kati ya Singida FG na Simba saa 2:15 kwenye uwanja wa New Amaan Complex.

Singida imeingia hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa Azam Katika hatua ya robo fainali huku Simba akiitoa Jamhuri.

Singida FG na Simba ndiyo wawakilishi pekee wa Ligi Kuu ya NBC waliobaki ndani ya michuano hii ya Mapinduzi baada ya Azam na Yanga kutolewa katika hatua ya robo faianali.