NBC CHAMPIONSHIP HAKUNA KULALA, MECHI TATU KUPIGWA LEO.

 

LIGI ya NBC Championship inaendelea leo januari 7, kwa michezo mitatu kupigwa kwenye mikoa mitatu tofauti.

Mkoani Mara Biashara United watakuwa wenyeji wa Mbuni saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Karume.

Mchezo huo unabeba hisia za mashabiki wengi kutokana na nafasi za kila timu, Biashara wapo nafasi ya tano kwenye msimamo wakiwa na alama 30 huku Mbuni ikiwa nafasi ya sita kwenye msimamo na alama 27 hivyo kila timu kupambana kutafuta alama tatu ili kusogea juu zaidi kwenye msimamo.

Ruvu Shooting watawaalika FGA Talents kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma saa 10:00 alasiri, Ruvu Shooting wapo nafasi ya mwisho kwenye msimamo wakiwa na alama mbili pekee baada ya kucheza michezo 15.

Mchezo wa mwisho hii leo utazikutanisha Cosmopolitan na Pamba kwenye uwanja wa Mabatini mkoani Pwani saa 10:00 alasiri.

Michezo hii inakwenda kukamilisha mzunguko wa 16 wa Ligi ya NBC Championship.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *