SIMBA WAENDELEZA UBABE DHIDI YA TABORA UNITED

Ligi Kuu ya NBC  ambayo ni Ligi ya nne kwa ubora barani Afrika imeendelea kwa mchezo mmoja uliochezwa mkoani Tabora ambapo timu ya Tabora United waliwakaribisha Simba katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Mchezo huo umeanza majira ya saa kumi alasiri kwa timu zote kucheza kwa tahadhari kwani mchezo huo ulitawaliwa na tambo za Tabora kuwafunga Azam uwanja wa Ali Hassan Mwinyi  na Yanga katika uwanja wa Azam Complex.

Dakika 12 ziliwatosha Simba kufungua akaunti ya mabao kupitia  mshambuliaji wao Leonel Ateba kisha dakika ya 34 kuongeza bao la pili kupitia mkwaju wa penati hivyo kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili .

Kipindi cha pili Simba walizidi kulisakama lango laTabora  licha ya timu hiyo kufanya mabadiliko kwa  wachezaji wawili  lakini Simba walikuwa wakicheza kwa kasi na ufundi mwingi dakika ya 67 beki wa Simba Shomari Kapombe aliongeza bao kwa timu yake akipokea pasi kutoka kwa Leonel Ateba  akififisha matumaini ya Tabora United kurejesha mabao hao.

Dakika 90 za mchezo huo zimetamatika kwa Simba kuendekeza ubabe  kwani tangu Tabora United wapande daraja hawajawahi kuwafungana leo wakiondoka na mabao matatu huku mchezaji  Leonel Ateba akitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Simba wamerejea kileleni wakiwa wamefikisha alama 43 wakifunga mabao 34 huku wakiruhusu mabao matano katika michezo 16 ya Ligi Kuu ya NBC waliyocheza .

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *