UTAMU wa Ligi Kuu ya NBC unazidi kukolea ambapo jana katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa mkoani Manyara timu ya Fountain Gate iliikaribisha timu ya Young Africans katika mchezo uliochezwa majira ya saa kumi jioni.
Katika mchezo huo timu zote zilianza kucheza kuwa kasi ili kuweza kupata alama tatu muhimu ambapo iliwachukua dakika 38 timu ya Young African kufungua ukurasa wa abao kupitia mshambuliaji wao Clement Mzize huku dakika ya 43 Kiungo wa timu hiyo Aziz Ki akiongezea bao la pili hivyo kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza 0-2.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Fountain Gate wakitafuta nafasi ya kusawazisha ambapo hatahivyo ndoto zao zilizimwa baada ya dakika ya 70 Clement Mzize kuongeza bao la tatu huku Clatous Chama akiweka bao la nne dakika ya 89 hivyo mchezo kutamatika kwa matokeo ya 0-4.
Mchezaji wa Young Africans,Clement Mzize alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo.