Category: STORY

YANGA YAMALIZA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA MAPINDUZI NA SULUHU.

 

Mwakilishi wa Ligi Kuu ya NBC Yanga amemaliza michezo yake ya hatua ya makundi ya Kombe la Mapinduzi kwa suluhu dhidi ya KVZ.

Yanga amemaliza kinara wa kundi C baada ya kushinda michezo miwili na kupata sare mchezo mmoja hivyo kufikisha jumla ya alama saba ambazo hakuna timu katika kundi hilo ambayo inaweza kufikia alama hizo.

Baada ya matokeo hayo Yanga anafuzu moja kwa moja katika hatua ya Robo fainali ya Kombe hilo linaloendelea kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

YANGA KUIPEPERUSHA BENDERA YA LIGI KUU YA NBC KOMBE LA MAPINDUZI LEO.

 

KOMBE la Mapinduzi linaendelea leo huko Visiwani Zanzibar, saa 2:15 usiku wawakilishi wengine wa Ligi Kuu ya NBC Yanga watakukatana KVZ katika mchezo wa mwisho wa kundi C.

Yanga wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama sita baada ya michezo miwili huku KVZ wakiwa na alama nne baada ya michezo miwili.

Jana mchezo wa wawakilishi wawili wa Ligi kuu ya NBC Simba dhidi ya Singida FG ulimalizika kwa simba kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri, mabao ya Simba yalifungwa na Willy Onana na Luis Miquissone.

SIMBA, SINGIDA FG NI VITA YA LIGI KUU YA NBC NDANI YA MAPINDUZI CUP

 

KOMBE la Mapinduzi linaendelea leo visiwani Zanzibar kwa mchezo wa ‘miamba’ ya Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba na Singida Fountain Gate saa 2:15 katika uwanja wa New Amaan Complex.

Simba na Singida FG wapo Kundi B katika michuano hiyo ya Mapinduzi ambapo Simba ana alama 3 baada ya kucheza mchezo mmoja huku Singida FG akiwa na alama 6 baada ya kucheza michezo miwili na kushinda yote.

Mchezo huo unawakutanisha wawakilishi wawili kati ya wanne wa Ligi Kuu ya NBC katika Kombe hilo la Mapinduzi

KMC, TABORA UTD KUZIKABILI SIMBA NA YANGA LIGI KUU YA NBC LEO.

 

MCHAKAMCHAKA wa Ligi Kuu ya NBC unaendelea tena leo kwa michezo miwili ya ‘kibingwa’ kwenye mikoa miwili tofauti.

Saa 10:00 alasiri KMC wataialika Simba katika uwanja wa Azam Complex mkoani Dar es salaam.

KMC itatumia uwanja wa Azam Complex kama uwanja wao wa Nyumbani baada ya uwanja wa Uhuru kuwa katika marekebisho.

Tabora United watakuwa wenyeji wa Yanga katika uwanja Jamhuri mkoani Dodoma saa 1:00 usiku.

Tabora United wanatumia uwanja wa Jamhuri, Dodoma kama uwanja wao wa nyumbani badala ya Ali Hassani Mwinyi licha ya kufunguliwa, hii ni kwasababu uwanja huo upo katika uangalizi wa siku saba tangu ulipofunguliwa Desemba 21, kama kanuni ya Ligi Kuu toleo la 2023 inavyoelekeza.

AZAM HAIKAMATIKI, TANZANIA PRISONS, GEITA ZATAKATA LIGI KUU YA NBC.

LADHA ya Ligi Kuu ya NBC iliendelea leo kwa michezo mitatu iliyochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti.

Saa 8:00 mchana Tanzania Prisons walikua wenyeji wa Namungo katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Tanzania Prisons kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Samson Mbangula dakika ya 42 ya mchezo.

Saa 10:00 jioni Geita Gold waliwaalika Singida FG katika uwanja wa Nyankumbu na Geita kuibuka na ushindi wa bao 1 likifungwa na Mchezaji Valentino Mashaka Kusengama dakika ya 79 ya mchezo.

Mchezo wa mwisho ulizikutanisha Kagera Sugar dhidi ya Azam katika uwanja wa Kaitaba Mkoani kagera na kumalizika kwa Kagera Sugar kukubali kichapo cha mabao 4-0.

Kwa matokeo haya Azam anazidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC akifikisha jumla ya alama 31 huku akiwa amecheza michezo 13 tofauti ya alama nne na Yanga anayeshika nafasi ya pili huku akiwa amecheza michezo 10 .