Ligi Kuu ya NBC inatarajiwa kurejea tena Februari 1, 2025 kwa mchezo mmoja kati ya Young Africans na Kagera Sugar saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa KMC Complex.
Mpaka Ligi inasimama Desemba 29, 2024 jumla ya mabao 266 yalifungwa huku Mchezaji Elvis Rupia wa Singida Black Stars akiongoza kwa ufungaji akiwa na mabao nane akifuatiwa na Jean Ahoua wa Simba akiwa na mabao 7.
kwa Upande wa pasi za mabao Feisal Salum wa Azam FC anaongoza kwa kutoa pasi za mabao tisa akifuatiwa na Jean Ahoua wa Simba na Salum Kihimbwa wa Fountain Gate wote wakiwa na pasi za mabao matano.
Mlinda Mlango wa Simba Moussa Camara anaongoza kwa upande wa hati safi (Clean sheets) akiwa nazo 12 akifuatiwa kwa karibu na Patrick Munthali wa Mashujaa mwenye ‘Clean Sheets’ nane wakifuatiwa na Metacha Mnata wa Singida Black Stars na Djigui Diarra wa Young Africans wenye ‘Clean sheets’ saba kila mmoja.
Jedwali hapo chini limejumuisha wachezaji wote waliohusika kwenye ufungaji na utengenezaji wa mabao sambamba na walinda milango wote wenye hati safi ‘Clean sheets’.



















