RAIA wa Misri Amin Mohamed Amin ndiye atakayechezesha mchezo wa Young Africans dhidi ya Simba maarufu kama ‘Kariakoo Dabi’ Juni 25 kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Ikiwa Yanga itashinda mchezo huo au kutoa sare ya aina yoyote itaibuka mshindi wa kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 na ikiwa Simba itafanikiwa kushinda itaibuka mabingwa wapya wa kombe hilo.
Amin atasaidiwa na Mahmoud El Regal,Samir Gamal Mohamed na Ahmed Mahrous Elghandour wote kutoka nchini Misri huku mtathimini waamuzi akiwa ni Alli Mohamed kutoka nchini Somalia.
Hii ni mara ya kwanza kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kusimamiwa na waamuzi wa mchezo kutoka nje ya Tanzania.
Mchezo huo ambao mwenyeji ni timu ya Young Africans yenye alama 79 huku ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Simba yenye alama 78 ikishika nafasi ya pili utapigwa saa kumi na moja jioni.
Ni bora sana kuchukua marefa kutoka nje, mechi za dabi ya kariakoo simba vs yanga ili kuondoa utata maana washabiki huwa na mashaka na marefa wazawa.