Category: STORY

AHOUA ‘HACHEKI NA WOWOTE’ LIGI KUU NBC.

JEAN Ahoua wa timu ya Simba ameendelea kuwa na msimu bora wa Ligi Kuu ya NBC hadi sasa baada ya kuhusika kwenye mabao 19 huku timu yake ikisalia na michezo nane kutamatisha msimu.

Ahoua aliyesajiliwa na Simba akitokea Asec Mimosa mpaka sasa amehusika katika mabao 19  baada ya kufanikiwa  kufunga mabao 12 kutoa pasi zilizozaa mabao saba hivyo kufanya kuwa mchezaji aliyehusika katika mabao mengi kuliko mchezaji yeyote.

Prince Dube  ambaye amesajiliwa  na timu ya Young Africans akitokea Azam  anashikilia nafasi ya pili akiwa amehusika katika mabao 17 baada ya kufunga mabao 10 na kutoa pasi za mabao saba.

Mpinzani wa karibu wa Dube ni Feisal Salum wa Azam akiwa amefanikiwa kutoa pasi za mwisho 12 na kufunga mabao manne  hivyo kuhusika katika mabao 16.

Kwa upande wake Aziz Ki wa Young Africans amefanikiwa kufunga mabao saba na kutoa pasi za mabao saba hivyo kuhusika katika mabao 14.

Pacome Zouzoua na Clement Mzize wa Young Africans wote wamehusika katika mabao 13 kila mmoja  huku Pacome akifunga mabao saba na kutoa pasi za mwisho sita huku Mzize akifunga mabao 10 na kutoa pasi za mwisho tatu.

NANI KUMFUATA HAUSUNG NBC CHAMPIONSHIP

NANI KUMFUATA HAUSUNG NBC CHAMPIONSHIP ?

NANI kuungana na Hausung kwenye Ligi ya Championship ya NBC ndiyo swali linalosubiri majibu yake kutoka kundi B la First League ambapo Rhino Rangers, Gunners na Tanesco wanayo nafasi ya kufanya hivyo.

Rhino Rangers ya Tabora ina Jumla ya alama 31 kwenye michezo 13 huku Gunners ya Dodoma ikiwa na alama 29 kwenye michezo 12 wakati Tanesco ya Morogoro ikiwa na alama 26 kwenye michezo 26.

Ikumbukwe kuwa timu inayoshika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa First League Kundi A na B Inafuzu moja kwa moja kushiriki Ligi ya Championship ya NBC.

Wakati timu zinazoshika nafasi ya pili na ya tatu kwenye kila kundi zikicheza michezo ya mtoano (PlayOff) kupata washindi wawili wa kucheza mtoano wa kupanda (Promotion PlayOff) na timu mbili za ligi ya Championship ya NBC.

NBC CHAMPIONSHIP YAZIDI KUNOGA

Ligi ya Championship ya NBC mzunguko wa 24 umemalizika kwa Mtibwa Sugar kuwa kinara ikiwa na alama 57 na kushika nafasi ya kwanza huku ikifunga mabao 47 na kufungwa mabao 34.

Nafasi ya pili inashikwa na Mbeya City yenye alama 52 mabao 48 huku ikifuatiwa na Stand United inayoshika nafasi ya tatu na alama 52 ikifunga mabao 40.

Geita Gold inashika nafasi ya nne ikikusanya jumla ya alama 48 baada ya kufunga mabao 41 na kufungwa 22.

Timu hizi nne zipo kwenye ushindani mkubwa wa kugombea nafasi ya kucheza Ligi Kuu ya NBC msimu ujao zikipishana kwa tofauti ya alama chache kwenye msimamo.

MANUNGU TISHIO KWA TIMU NGENI NBC CHAMPIONSHIP.

UWANJA wa Manungu uliopo Mkoani Morogoro umekuwa tishio kwa timu zinazoenda kucheza dhidi ya mwenyeji wa uwanja huo Mtibwa Sugar baada ya timu hiyo kushinda michezo 12 hadi sasa kwenye uwanja huo na kuwa idadi kubwa hadi sasa kwenye Ligi ya NBC Championship.

Mtibwa iliongeza idadi ya ushindi wikiendi iliyopita baada ya kutoka nyuma dhidi ya Biashara United iliyokuwa ikiongoza 2-0 kipindi cha kwanza na Mtibwa kumaliza mchezo kwa ushindi wa 3-2.

Uwanja wa Kambarage unaotumiwa na Stand United unashika nafasi ya pili baada ya timu mwenyeji wa uwanja huo Stand United kushinda michezo 11 hadi sasa huku idadi hiyo ikitimia baada ya Stand kushinda mchezo uliopita kwa mabao 3-0 dhidi ya African Sports ya Tanga.

Nyankumbu, Geita uwanja unaotumiwa na Geita Gold unafuata baada ya Geita kushinda michezo 11 idadi sawa na Stand inayotumia uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

HAUSUNG RASMI LIGI YA CHAMPIONSHIP YA NBC

TIMU ya Hausung kutoka Makambako mkoani Njombe imekuwa timu ya kwanza kupanda daraja kwenda Ligi ya Championship ya NBC kutoka kundi A la First League.

Hausung wenye alama 25 huku wakiwa wanaongoza kundi A wamefanikiwa kupanda daraja baada ya kucheza  michezo 13 kati ya 14 ambayo wanapaswa kucheza.

Mbali na alama hizo Hausung wamefanikiwa kufunga mabao 19 huku wakiruhusu mabao 11 katika michezo 13 huku wakiwa wameshida michezo saba wakitoka sare michezo minne na kufungwa mechi nne.

Nyumbu wapo nafasi ya pili katika msimamo huo wakiwa na alama 21 baaba ya kucheza michezo 13 wakishinda michezo sita,wakipata sare tatu na kufungwa michezo minne  huku ukibaki mchezo mmoja ligi hiyo ambao hata kama wakishinda hawataweza kufikia alama ambazo timu ya Hausung  imeweza kuzikusanya.