Category: STORY

LIGI KUU YA NBC KUENDELEA LEO, MASHUJAA KUJIULIZA KWA SIMBA.

 

LIGI Kuu ya NBC inaendelea leo Februari 3 kwa mchezo mmoja kupigwa mkoani Kigoma.

Mashujaa itaikaribisha Simba kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma saa 10:00 alasiri.

Mashujaa inaingia kwenye mchezo huu ikiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo ikijikusanyia alama tisa kwenye michezo 12 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na alama 23 kwenye michezo 10.

NBC CHAMPIONSHIP KUPIGWA MIKOA SITA LEO.

 

LIGI ya NBC Championship mzunguko wa 20 unaanza leo Februari 3 kwa michezo sita kupigwa kwenye mikoa sita tofauti.

Mchezo wa mapema saa 8:00 mchana utazikutanisha Stand United dhidi Biashara United kwenye uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Mkoani Mbeya KenGold itaikaribisha Mbeya City saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Sokoine huku KenGold ikiingia kwenye mchezo huu ikiwa kinara kwenye msimamo na alama 43 kwenye michezo 19 huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 7 na alama 32 kwenye michezo 19.

Mkoani Arusha ni “ Derby ya Jeshi” kati ya Mbuni na TMA saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku alama moja pekee ikiweka utofauti baina ya timu hizi TMA ikiwa nafasi ya nne na Alama 37 huku Mbuni ikiwa nafasi ya tano na alama 36 hivyo kuufanya mchezo huu kuwa wa kuvutia.

Mchezo mwengine utazikutanisha FGA Talents dhidi ya Polisi Tanzania saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Mkoani Mwanza Copco itaikabili Pamba kwenye uwanja wa Nyamagana saa 10:00 alasiri mchezo huu ukiwa ‘Mwanza Derby’ kutokana na timu zote kutokea mkoa wa Mwanza.

Mchezo wa mwisho utapigwa mkoani Pwani Pan African itaikabili Cosmopolitan kwenye uwanja wa Mabatini saa 10:00 alasiri.

KAGERA SUGAR, YANGA HAKUNA MBABE.

 

LIGI KUU ya NBC imerejea leo kwa mchezo mmoja uliopigwa kati ya kagera Sugar na Yanga katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera na kumalizika kwa suluhu.

Kwa matokeo haya Kagera Sugar inapanda kwa nafasi moja kutoka 14 hadi 13 baada ya kufikisha alama 14 kwenye michezo 14 huku Yanga ikiendelea kusalia nafasi ya 2 ikiwa na alama 31 kwenye michezo 12.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mchezo mmoja kati ya Mashujaa na Simba kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

LADHA ZA LIGI KUU YA NBC KUREJEA LEO.

 

LIGIKUU ya NBC inarejea leo Februari 2 baada ya kusimama kwa takribani siku 40 kupisha fainali za mataifa ya Afrika.

Mchezo mmoja utapigwa leo Kagera Sugar ikiikaribisha Yanga kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera saa 10:00 alasiri.

Kagera Sugar inaingia kwenye huu mchezo ikiwa nafasi ya 14 kwenye msimamo baada ya kukusanya alama 13 kwenye michezo 13 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili baada ya kujikusanyia alama 30 kwenye michezo 11.

Kagera inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wake uliopita wa Ligi Kuu ya NBC kwa mabao 4-0 dhidi ya Azam nyumbani huku Yanga ikishinda mchezo wake uliopita kwa bao 1 lililofungwa na Stephane Aziz Ki dhidi ya Tabora United ugenini.

‘STAA’ YUPI WA LIGI KUU YA NBC KUMFUATA INONGA ROBO FAINALI LEO ?

KOMBE la Mataifa ya Afrika linaendelea nchini Ivory Coast huku ‘Mastaa’ watatu wa Ligi Kuu ya NBC wakisalia hadi sasa kwenye mashindano hayo.

Mashindano hayo yanaendelea leo huku wachezaji wawili wa Yanga Djigui Diarra anaekipiga timu ya taifa ya Mali na Stephane Aziz Ki wa Burkina Faso wakikutana leo kila mmoja akitafuta nafasi ya kucheza robo fainali.

Tayari ‘staa’ mmoja wa Ligi Kuu ya NBC Henock Inonga anaecheza timu ya Simba ameshafuzu hatua ya robo fainali kwenye mashindano yake na timu ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuitoa timu ya Misri.

Mshindi wa mchezo wa leo kati ya Diarra na Ki Aziz ndiye atasalia kwenye mashindano hayo na atakayepoteza atarejea nchini kuitumikia timu yake kwenye michezo ya Ligi Kuu ya NBC inayotarajiwa kurejea Februari 2 kwa mchezo kati ya Kagera Sugar dhidi ya Yanga.