Category: STORY

‘LADHA’ ZA LIGI KUU YA NBC KUREJEA LEO

LIGI Kuu ya NBC inarejea Leo Novemba 22 kwa michezo miwili baada ya kusimama kwa siku 13 kupisha kalenda ya FIFA ya michezo ya kimataifa.

Mchezo wa kwanza utazikutanisha Geita Gold inayoshika nafasi ya 15 ikiwa na alama saba dhidi ya JKT Tanzania inayoshika nafasi ya sita ikiwa na alama 14 katika mchezo utakaoanza saa 10:00 alasiri katika uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.

Mchezo wa mwisho hii leo utazikutanisha Kagera Sugar inayoshika nafasi ya nane ikiwa na alama 12 dhidi ya KMC iliyo na alama 15 kwenye nafasi ya tano, saa 1:00 usiku kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

RUVU KUJIULIZA KWA STAND , MBUNI, POLISI VITA NBC CHAMPIONSHIP LEO

Ligi ya NBC Championship inaendelea leo Novemba 17 kwa michezo miwili kwenye mikoa miwili tofauti.

Mchezo wa saa 8:00 Mchana Stand United watawaalika Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Stand ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo ikicheza jumla ya michezo 10 na kupata ushindi kwenye michezo mitatu, sare tatu na kufungwa minne huku ikikusanya alama 12.

Ruvu Shooting ipo nafasi ya mwisho kwenye msimamo baada ya kucheza jumla ya michezo 10 ikifungwa michezo 9 na kupata sare mchezo mmoja ikiwa haijashinda mchezo wowote na kuwa na alama moja.

Mchezo wa pili utazikutanisha Mbuni dhidi ya Polisi Tanzania saa 10:00 alasiri katika uwanja wa Black Rhino, Karatu.

Mbuni ipo nafasi ya nne ya Msimamo baada ya kucheza michezo 10 na kushinda mitano wakitoa sare mitatu na kufungwa miwili huku wakikusanya Alama 18 na Polisi wakishika nafasi ya sita kwenye msimamo ikicheza jumla ya michezo 10 ikitoa sare michezo miwili na kufungwa michezo mitatu na kuwa na jumla ya alama 17.

TMA WABABE WA FIRST LEAGUE WANAOTESA NBC CHAMPIONSHIP.

 

Timu ya TMA yenye maskani yake Arusha inayoshiriki ligi ya NBC Championship imekua na mwanzo mzuri ndani ya ligi hiyo hadi hivi sasa huku ikishiriki ligi hiyo kwa msimu wa kwanza.

TMA ndio timu pekee kwenye Ligi ya NBC Championship ambayo haijapoteza mchezo wowote wa ligi hiyo hadi sasa.

Timu hiyo ambayo imepanda daraja msimu huu kutoka First League imekuwa na mwenendo mzuri baada ya kucheza jumla ya michezo tisa ikishinda michezo sita na kwenda sare michezo mitatu.

MASHUJAA, GEITA KUSAKA HESHIMA LIGI KUU NBC

LIGI KUU ya NBC inaendelea leo Novemba 6 kwa michezo miwili kwenye Mikoa miwili tofauti kati ya Mashujaa wakiwaalika Singida BS kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani kigoma na Geita Gold dhidi ya Tabora United kwenye uwanja wa Nyankumbu, Geita huku michezo yote ikianza saa 10:00 alasiri.

Mashujaa wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza michezo mitatu mfululizo ya Ligi Kuu ya NBC.

Geita Gold inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo minane ikishinda mmoja, ikisuluhu michezo mitatu na kufungwa mitano hivyo kukusanya alama sita.

Tabora United ipo nafasi ya nane ikishinda michezo miwili,
sare michezo minne na kufungwa mitano hivyo kuwa na alama 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

YANGA YAIADHIBU SIMBA LIGI KUU YA NBC.

MABAO 5-1 walioshinda Yanga dhidi ya Simba yametosha kuwabakiza kileleni mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya NBC kwa alama 21 baada ya kucheza mechi tisa.

Mabao yaliyofungwa na Kennedy Musonda, Maxi Nzengeli aliyefunga mawili, Ki Aziz na Pacome Zouzoua yameifanya Simba kuruhusu mabao 10 huku wakifunga 17.

Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha jumla ya mabao 25 kwenye michezo 9 waliyocheza mpaka sasa.

Yanga wamesalia kileleni mwa msimamo wakiwaacha wapinzani wao Simba na pointi zao 18 huku Simba wakiwa wamecheza mechi saba .